Ticker

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

Responsive Advertisement



MAONI YANGU KUHUSU MABADILIKO YA KATIBA

 Nadhani ingependeza kama nasi huku ughaibuni tungekuwa tunabadilishana mawazo kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya katiba(INGAWA KUNA WALE WANAOAMINI KUWA HATUNA TUNACHOWEZA KUBADILISHA.KILA KITU KIMESHAAMULIWA NA WAKUU WENYE SAUTI TANZANIA).
Mimi nilishayapeleka yangu www.katiba.go.tz.Na kama wengi wetu hawana wakati wa kueleza mengi , ni bora tujaze hili suala la URAIA PACHA Bila ya sisi huku ughaibuni kulipigia debe, huenda na wale wa nyumbani hata wasilikumbuke.
Maoni yangu yana sehemu nne kuu zifuatazo:

1. KINGA YA RAISI .


Anapokuwa madarakani asishtakiwe ila mara tu muhula wake wa kuongoza unapokwisha na siku anapoapishwa Raisi mpya,KINGA ya Raisi mstaafu ifutike automatically ili aweze kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.Na ikipita miaka mitano tangu kumaliza uongozi na akawa hakushtakiwa kwa kosa lolote ,Kinga yake arudishiwe na kuanzia hapo hatoweza tena kushtakiwa.
(UCHAMBUZI )Viongozi wengi wa Afrika wanatumia vibaya mno madaraka yao wakijijua kuwa hawatoshtakiwa wanapotoka madarakani.Kuwepo kipengee hiki kutasaidia wapunguze ubadhirifu wanapokuwa madarakani.

2. WAFUNGWA:


a) HUKUMU YA KIFO ISIWEPO. Kwa kosa lolote HATA LA KUUA AU LA UHAINI.Hukumu ya juu iwe ni kifungo cha maisha.
(UCHAMBUZI )Tunapomuua tunakuwa tumempumzisha na wala hatohisi uchungu wa adhabu kwa lile kosa alilofanya.Mimi hapa wala silalii katika ile hoja ya HAKI YA MWANADAMU KUISHI wanayoitumia baadhi ya wale wanaopinga hukumu ya kifo duniani.
b)KITUMIKE KIFUNGO CHA NJE NA KAZI ZA KUNUFAISHA JAMII kwa makosa yasiyokuwa ya jinai,
(UCHAMBUZI ) Ndugu zetu wengi hupelekwa rumande kwa kuiba kuku na wanapotakiwa watoe dhamana wanashindwa na hurundikwa rumande na nchi hulazimika kuwahudumia bila faida yoyote.Kinachosikitisha wengi wanaokwenda rumande ni hawa ndugu zetu masikini wakati wale wenye uwezo wa kiuchumi (na hasa wageni)hulipa kiwango chochote wanachotakiwa na wanakuwa na uhakika wa kutokwenda jela.!!
c)IFUTWE CRIMINAL RECORD baada ya kupita miaka kumi tangu mfungwa kumaliza kifungo chake bila kufanya kosa jingine la jinai.
(UCHAMBUZI) Wafungwa wanapomaliza kifungo huwa wanabaki maisha yao yote katika records za INTERPOL kuwa ni criminals, na hii inawakosesha haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika jamii yao au hata kupata kazi kwa kuwa huonekana ni criminals.Hali hii inawafanya wengi warudie tena katika uharamia kwa sababu wanajihisi kuwa jamii haiwapi nafasi ya kubadilisha au kuifuta sifa mbaya ya u -crimial inayowaandama maisha yao yote kutokana na justice system ilivyo ya kidhuluma na uonevu duniani.



3. MUUNGANO:

Kuwe na nchi inayoitwa ZANZIBAR ,
Kuwe na nchi inayoitwa TANGANYIKA (au jina lolote litalochaguliwa)
Kuwe na mfumo wa Muungano utaokubalika na pande zote mbili( Kazi hii tuwachie wataalamu siyo kila mtu anaiweza).

4. URAIA PACHA(DUAL CITIZENSHIP)

Raia waruhusiwe kuwa na uraia pacha
(UCHAMBUZI) Hapa sina haja ya kuchambua kwa sababu zinaeleweka wazi faida za uraia pacha na mifano ipo wazi kwa zile nchi zenye mfumo huu jinsi zinavyofaidika katika kila nyanja.HAKUNA hasara wala madhara ya kuwa na uraia pacha zaidi ya faida tu.

KAYU LIGOPORA
ATHENS

Post a Comment

0 Comments